Description
Unapokuwa unauza au kuiongelea biashara yako,
Unakutana na maneno kama “bei ni kubwa”, “nitafikiria”, “sina pesa”, au “nitarudi baadaye”…na wakati mwingine unakosa la kusema au mteja anapotea kabisa?
VIPINGAMIZI NA NAMNA YA KUVIJIBU (Basic Objection Handling) ni kitabu kinachokusaidia kugeuza kila kipingamizi kuwa hatua ya kukusogeza karibu na mauzo au usajili.
Ndani yake utajifunza jinsi ya kuelewa chanzo halisi cha pingamizi la mteja,
Namna ya kujibu bila kubishana au kumfanya ajihisi kushinikizwa, na…
Mbinu za kuendeleza mazungumzo hadi mteja achukue hatua.
Pia utaelewa misemo na njia za kujibu zinazofanya mteja aendelee kusikiliza badala ya kukukataa.
Hiki si kitabu cha majibu ya kukariri, ni mwongozo unaokupa uelewa wa akili ya mteja na jinsi ya kuzungumza naye kwa namna inayojenga uaminifu na kuongeza uwezekano wa kufunga mauzo.
Baada ya kukisoma, utaanza kuwa na ujasiri zaidi kwenye mazungumzo, utaacha kupoteza wateja kwa vipingamizi vidogo, na utaongeza kiwango chako cha kufunga mauzo kwa urahisi zaidi.
Kama unataka vipingamizi visiwe kikwazo tena kwenye biashara yako, kitabu hiki kitakupa silaha sahihi ya kuvishinda.




Reviews
There are no reviews yet.