Jinsi tabia yako ya uso inavyopoteza wateja kimya kimya

Wateja wengi hawakimbii bidhaa…wanakimbia uso wa mfanyakazi.

Utafiti wa Worcester Polytechnic Institute (2018) uligundua kuwa karibu 55% ya mawasiliano ya mteja huathiriwa moja kwa moja na lugha ya mwili yaani body language, si maneno. Hii ina maana uso wako pekee unaweza kuamua kama mauzo yatafanyika au la.

Ukionekana umechoka, huna hamu, au hujapendezwa, mteja anatafsiri kama “sijakaribishwa hapa.”

Katika sekunde chache za kwanza, uso wako unatangaza huduma yako kabla hata hujaongea.

Suluhisho ni rahisi…kuwa na tabasamu la kawaida, macho ya umakini, na uso wa “wewe ni muhimu hapa.”

Mteja huamini uso wako kabla ya kuamini maneno yako.

Kwa uhitaji wa mafunzo ya utoaji huduma bora kwa wateja tuwasiliane kwa kupiga 0683911049

Naitwa Coach Lazaro Samwel

 

Responses

Your email address will not be published. Required fields are marked *