Description
Unawahi kuhisi kuna mambo mengi kwenye maisha unayaona hayako sawa… lakini kila mtu anajifanya kama ni kawaida?
UKWELI USIOPENDA KUUSIKIA
Ni kitabu kinachovunja ukimya kwa kusema wazi yale ambayo wengi wanayajua moyoni lakini wanaogopa kuyasema hadharani, kuhusu elimu, mahusiano, biashara, na maisha kwa ujumla.
Ndani yake utakutana na mitazamo tofauti inayotikisa fikra ulizozoea, ikikuonyesha kwa nini baadhi ya “kanuni za kawaida” ulizofundishwa zinaweza kuwa zinakuzuia kufikia mafanikio.
Kitabu hiki hakikubembelezi, kinakupa ukweli halisi, unaoweza kukuumiza kidogo, lakini ndio unaoweza kukuamsha na kukusukuma kuchukua hatua sahihi.
Baada ya kukisoma, utaanza kuona maisha kwa jicho tofauti, utaweza kuchuja ushauri usio na msaada, kufanya maamuzi kwa uhuru zaidi, na kuacha kuishi kwa kufuata mitazamo ya watu bila kuhoji.
Utajijengea ujasiri wa kufikiria kwa kina, kuhoji, na kuchukua hatua zinazokuletea matokeo halisi.
Hiki ni kitabu kwa ajili yako kama uko tayari kusikia ukweli… na kuutumia kubadilisha maisha yako.





Reviews
There are no reviews yet.