Description
Unajitahidi kuuza bidhaa zako…lakini…
Unaposema moja kwa moja watu hawavutiki, wanapuuza au wanakuona kama unawaomba wanunue?
UZA BIDHAA ZAKO KWA HADITHI ni kitabu kinachokusaidia…
Kubadilisha namna unavyouza, kutoka kuuza kwa maelezo ya kawaida hadi kuuza kwa njia inayogusa hisia na kuvuta uamuzi wa mteja bila shinikizo.
Â
Ndani yake utajifunza jinsi ya kutumia hadithi kuonyesha tatizo la mteja bila kumkemea,
Namna ya kumwongoza mteja kuona suluhisho kupitia bidhaa yako, na jinsi ya kuwasilisha ujumbe unaomfanya ajione mwenyewe akihitaji kununua.
Pia utaelewa muundo wa hadithi zinazouza na jinsi ya kuzitumia kwenye mazungumzo, WhatsApp, na mitandao ya kijamii.
Hiki si kitabu cha storytelling ya burudani…ni mwongozo wa vitendo wa kubadilisha hadithi zako kuwa chombo cha mauzo kinachofanya kazi kila siku.
Baada ya kukisoma, utaanza kuona watu wakivutiwa zaidi na ujumbe wako, utaongeza kiwango cha majibu kutoka kwa wateja, na utaanza kuuza kwa urahisi zaidi bila kuhisi kama unalazimisha mtu.
Kama unataka bidhaa zako zianze kununuliwa kwa sababu ya jinsi unavyoeleza, si kwa sababu unalazimisha, kitabu hiki kitabadilisha kabisa mchezo wako wa mauzo.




Reviews
There are no reviews yet.